Menu

Pretoria, Afrika Kusini

Washiriki: Ahmed Kathrada – Mwasisi wa  Ahmed Kathrada Foundation, Ela Gandhi – aliyekuwa Mbunge wa, Jamuhuri ya Afrika Kusini , Jaji  Yvonne Mokgoro – alikuwa Jaji wa Mahakama  ya Kikatiba ya Afrika Kusini, Sizwe Mpofu-Walsh – Mwasisi Mwenza wa  InkuluFreeHeid, Frederik T. de Ridder – Mkurugenzi mkuu wa InkuluFreeHeid.

Maelezo Zaidi: Ili kuadhimisha kumbukumbu za miaka 50 za kesi za  Rivonia ambazo zilisababisha kufungwa kwa Nelson Mandela na Ahmed Kathrada, huu ulikuwa ni mkutano wenye mtindo wa ukumbi wa mjini kuhusu ujengaji amani na maridhiano , ambao ulihudhuriwa na viongozi kutoka kwenye jumuia nzima, ambao walikuja pamoja kwenye kikao ambacho mada yake ilikuwa ‘Nani utakayeridhia naye amani?’'

Ufuatao ni utangulizi wa Video wa Vipindi vya Moja kwa moja wa Ulimwenguni kote

Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Mwenyekiti Wa: UNICEF

Maelezo Zaidi: kutoka Goma, wawakilishi kutoka  UNICEF walikuja pamoja katika sehemu ya utangazaji wa masaa 24 wa Ulimwenguni kote kuhusu siku ya amani ili kuweza kuzungumzia namna ambavyo siku ya amani inavyoweza kusaidia shughuli zao za kuokoa maisha pamoja kwa mada: Nani utakayeridhia naye amani?

The Hague, Uholanzi (Kampuni)

Mwenyekiti Wake: Jeremy Gilley – Mwasisi wa Peace One Day

Washiriki: Howard G. Buffett – Kamati ya Wakurugenzi, Kampuni ya Coca-Cola Company na Mwasisi wa Wakufu wa Howard G. Buffett, Richard Reed – Mwasisi- Mwenza wa of Innocent Drinks, Peter Dahlström - Mkurugenzi, McKinsey & Company, Michael Mapes – Rais wa Flexible Products & Services, GREIF, Tanguy de Ripainsel – Meneja Mkuu wa Meneja wa Dior Uholanzi.

Maelezo Zaidi: Safari ya Peace One Day katika kuanzisha na kurasimisha siku ya kila mwaka ya kusitisha vita na kutokuwa na ukatili- Siku ya Amani, imepata msaada wa kipekee kutoka kwenye sekta ya kampuni. Muda huu wa Ulimwenguni kote umeweza kuleta pamoja wale wanaounga mkono Peace One Day kutoka kwenye sekta ya kampuni ya makampuni ili kuweza kuzungumza wajibu wa sekta ya makampuni katika mchakato wa amani na namna ambavyo Peace One Day inaweza kutumia nguvu na mshikamano huu katika kukuza zaidi kuhusu siku hii kwenye miaka ijayo.

 

The Hague, Uholanzi – Ukatili Wa Nyumbani

Mwenyekiti wake: Jeremy Gilley – Mwasisi wa Peace One Day

Washirirki: Baroness Scotland QC – Mwasisi na Wakufu ya Kukomesha Ukatili wa Nyumbani Ulimwenguni kote, Monique Coleman - Balozi wa Elimu wa Peace One Day  na Bingwa wa Vijana wa Umoja wa Mataifa, Marja Ruotanen – Mkurugenzi wa  Justice and Human Dignity Directorate, Council of Europe, Laura Bates – Mwasisi wa Everyday Sexism Project,  Dariusz Grzemny – Mfanyakazi wa Vijana, Vuguvugu la No Hate Speech Movement, Madi Sharma - Mjasiriamali wa kijamii na mwasisi wa kundi la Madi Group.

Maelezo zaidi: Baraza la Ulaya na vuguvugu la Hakuna Kauli ya Kuchukiza liliweza kuleta pamoja jopo la wataalam, wa wakilishi wa kiwango cha juu na vijana ili kuweza kuzungumzia masuala kuu yanayozungukia ukatili wa nyumbani na kuzungumzia hatua zinazochukuliwa katika kutatua masuala haya kote barani Ulaya na kwingineko.

Tokyo, Japani

Mwenyekiti Wake: Hiroki Sugiura – Mhariri mkuu katika Yokohama Keizai.

Washiriki: Tetra Tanizaki – Mwandishi wa TV na Redio ,Yukiko Kuroda – Mwasisi wa  People Focus Consulting / Kenji Sekine – Mwakilishi Mkurugenzi wa United for Peace Film Festival.

Maelezo Zaidi: Kikao hiki kiliyaleta pamoja mashirika ya chama cha kiraia, wawakilishi wa serikali na watu binafsi na mashirika kutoka katika sekta nyingine ili kuweza kuzungumzia umuhimu wa amani katika jumuia ya kisasa ya kijapani huku zingatio la kikao hiki likiwa Siku ya Amani.

Izraeli / Palestina

Mwenyekiti Wake: Shani Perez Kariv – Mwigizaji, Mkurugenzi na Mkurugenzi wa Kids Creating Peace.

Washiriki: Achinoam Nini – Mwimbaji, Mira Awad - Mwimbaji, Art Production Fund, Vijana Viongozi wakiwakilishi wa Kids Creating Peace

Maelezo Zaidi: Jopo hili liliimarisha mazungumzo kati ya washiriki waliokuwa wakiwakilisha Palestina na Izraeli na kuzungumzia namna ambavyo amani endelevu inaweza kuanzishwa kupitia katika kuwaleta watu binafsi na mashirika pamoja katika Siku ya Amani yenye mada: Nani utakayeridhia naye amani? Washiriki ambao walijumuisha wanamuziki, viongozi wachanga na wasanaii, waliweza kuchunguza wajibu wa elimu na mikutano ya mtu binafsi katika mchakato wa amani, haswa wakati wa kuiitenga na kujifanyia mambo yako.

Syria

Mwenyekiti Wake: SPARK

Maelezo Zaidi: 

'Amani ni kitu chenye thamani zaidi kwa binadamu'

Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 100,000 wamepoteza maisha yao katika mgogoro wa Syria, huku zaidi ya watu milioni1.7 wamelazimishwa kutafuta makazi katika nchi jirani. Kwenye Siku ya Amani, Peace One Day, iliweza kuwa na muda wa moja kwa moja Ulimwenguni kote kuanzia nchini Syria uliowaleta pamoja watu binafsi na mashirika ilikuweza kuzungumzia siku ya kila mwaka ya kusitisha vita na kutokuwa na ukatili ambayo ingeweza kuchangia katika kusitishwa kwa ukatili huu nchi nzima.

Medellín, Kolombia

Mwenyekiti Wake: Jeihhco – Kiongozi wa kijamii mwanaharakati na Mwasisi wa kundi la muziki wa kizazi  kipya  ‘Revolucion Sin Muertos’ (Ukombozi bila ya Maafa).

WashirikiPiedad Bonnett –Mwandishi, mwandishi wa riwaya na mshairi, Andrea Echeverri - Mwanamuziki na Mwasisi wa ‘Aterciopelados’ (Wale Mahameli), César López – Mwanamuziki na mwanaharakati wa kijamii. Muundaji wa ‘Escopetarra’ (gitaa ilioundwa kwa kutumia bunduki ishara ya maridhiano) na kiongozi wa wanzilishi ‘Toda Bala es Perdida’ (Kila risasi ni hasara), Aníbal Gaviria – Diwani wa Medellín, Vera Grave – Mwanaanthrolopojia, Mwasisi wa vuguvugu la vita vya msituni la M-19 ambalo sasa limeharamishwa na Mkurugenzi wa Observatorio para la PazSergio Ramírez – Mwandishi wa Kinikaragwa na mwandishi wa habari. Aliyekuwa Makamo wa Rais na mshiriki katika ukombozi wa  Sandinista. Alisaidia kuratibu mpito wa hadi demokrasia nchini Nikaragwa.

Maelezo Zaidi: Jiji la  Medellín liliweza kuwaleta pamoja watu binafsi na mashirika ya mseto mpana kuzungumzia masuala makuu yanayozungukia amani endelevu. Masuala haya yalijumuisha mijadala mikuu kuhusiana na kazi ya kujenga siku za usoni zenye amani zaidi katika jiji 

Melbourne, Australia

Mwenyekiti wake: Nic Frances Gilley MBE – Mjasiriamali wa kijamii na Balozi wa Peace One Day.

Washiriki: Tania Major – Mkurugenzi Mkuu, Tania Major Consulting Pty Ltd, Ellen Sandell – Mfanya kampeni wa kimazingira, Dr Nouria Salehi - Mwanafizikia wa Nuklia na mwanafizikia wa bayolojia

Maelezo Zaidi: Kulileta pamoja jopo pana, muda huu wa moja kwa moja Ulimwenguni kote uliweza kuunganisha chama cha Australia kwa jina la amani. Kwa kutumia Siku ya Amani kama zingatio washiriki waliweza kuzungumzia masuala makuu yanayozungukia mada ya Peace One Day mnamo mwaka 2013: Nani Utakaye Ridhia Naye Amani? Na namna  ambavyo sekta tofauti za chama cha Australia zinavyoweza kukuza ufahamisho wa siku ya Ulimwenguni kote ya kusitiisha vita nakutokuwa na - ukatili

Jiji la Meksiko, Meksiko

Washiriki: Sergio Kopeliovich – Mkurugenzi na mwasisi wa Journeys for Peace, Daniel Giménez Cacho - Mwigizaji, Javier Sicilia – Mkuu wa  Movimiento por la Paz con Justicia y Dignidad, Ernestina Sodi - Mwandishi.

Maelezo Zaidi: Kwa miaka na mikaka shughuli za kipekee zimefanyika kote Meksiko kwa kuunga mkono Siku ya Amani. Kipindi hiki cha Moja kwa Moja Ulimwenguni kote kilikuwa ni sehemu ya kampeni ya Peace One Day katika kuhamasisha hatua zaidi katika nchi hii kwenye Siku ya Amani. Sehemu ya hafla pana zaidi ya kitamaduni ambayo inajumuisha muziki, mashairi na hafla ya densi, kandobalkando ya mazungumzo ya kiwango cha juu ambayo yalizungumzia kuhusu masuala yanayozungukia haja ya amani. Washiriki walijumuisha waigizaji, watangazaji maarufu wa TV na viongozi wenye ushawishi mkubwa

New York, Marekani - Imani

Mwenyekiti Wake: Dr. William Vendley – Katibu Mkuu wa  Religions for Peace

Washiriki: Kinjal Dave – Kizazi Kijacho Kiongozi wa Seva wa Hindu American Seva Communities na Interfaith Youth Kiongozi Mkuu, Samantha Bloom. Kamati ya Uongozi wa Vijana katika Bodi ya Wakurugenzi kwa  Seeds of Peace na Ofisi ya Uhusishwaji ya Makampuni kwa ajili ya benki ya mataifa mbalimbali, Frank Fredericks – Mwasisi na Mkurugenzi Mkuu wa  World Faith na Mwasisi mwenza wa  Religious Freedom USA, Khalid Latif – Mkurugenzi wa  Islamic Center katika New York University na kasisi wa  New York City Police Department, Doyeon Park – Mwakilishi Mbadala wa Won Buddhism  katika  Umoja wa Mataifa na Mwekahazina wa Committee of Religious NGOs kwenye Umoja wa Mataifa, Simran Jeet Singh – Mkuu wa Dini wa  Sikh Coalition na Mwenyekiti wa Interfaith Committee for the World Sikh Council.

Maelezo Zaidi: Kukiwa na makadirio ya watu wazima na watoto wanadini wapatao bilioni 5.8 ulimwenguni kote, dunia yenye amani inawezekana tu pale ambapo imani za ulimwengu zitaweza kujapamoja kwa ushirikiano. Kipindi hiki cha Moja kwa Moja Ulimwenguni kote kiliweza kuwaleta pamoja jopo la viongozi wachanga, wakuu na waheshimiwa kutoka katika tamaduni mbalimbali za kidini, ambao walikuwa wameshughulika katika sekta mbalimbali za jamii. Washiriki waliweza kutafakari kuhusu wajibu wa kiroho katika maridhiano na uponyaji, na vilevile kuchunguza namna ambavyo siku ya kila mwaka ya amani inavyoweza kutumiwa na kizazi kipya cha waumini wa Kidini ili kuweza kushirikiana na kufaana wenyewe kwa wenyewe.

Brazil

Mwenyekiti Wake: Cid Blanco - Msimamizi wa Utamaduni Mawasiliano na hafla, mamlaka ya uma ya olimpiki (APO)

Washiriki: Virginia Garcez – Rais wa Chuo Kikuu cha Amani nchini Salvador,- Joselito Crispim – Kiongozi wa Jumuia , João Paulo Santos Gomes – Mkurugenzi wa "Filhos de Gandhy" (watoto wakiume wa Gandhy), Claudio Abdala – Katibu-saidizi wa ukarabati wa Ukumbi wa Jiji la  Salvador

Maelezo Zaidi: Kuleta pamoja jopo pana, kwenye kipindi hiki cha Moja kwa Moja Ulimwenguni kote kuliunganisha jumuia ya Brazil kwa jina la amani. Wakitumia Siku ya Amani kama zingatio, washiriki walizungumzia masuala makuu yanayozungukia mada ya Peace One Day ya mnamo mwaka wa 2013: Nani Utakayeridhia Naye Amani? Na namna ambavyo sekta tofauti za jumuia za Brazil zinavyoweza kukuza ufahamisho wa siku hii ya Ulimwenguni kote katika kusitisha vita na kutokuwa na ukatili.

Shanghai, China

Washiriki: Cookie Qian – Mwandishi, mwandishi wa  Lonely Planet China, Zhu Zhen – Mwasisi mwenza wa  Giftpi, Elvis Li – Mkurugenzi wa Biashara wa BBH China, Wynn Zhang- Meneja mkuuu wa Mauzo Diageo China, Li Ji – Mkurugenzi wa Filamu Vivian Chen -Msanii Ju Bai Yu – Mwandishi / Mhariri / Mwandishi wamakala

Maelezo Zaidi: Kipindi hiki cha Moja kwa Moja cha Ulimwenguni kote kilileta pamoja jopo pana la watu binafsi na mashirika ili kuzungumzia namna ambavyo ujumbe wa Siku ya Amani unavyoweza kuenezwa kote nchini. Kwa vile China ni nchi yenye idadi ya watu wengi zaidi ulimwenguni, msaada wa kutoka mashinani hapa ungekuwa wenye msukumo wakipekee katika kampeni ya kurasimisha siku hii.

Baghdad, Iraki

Mwenyekiti Wake: Umoja wa Mataifa nchini Iraki

Washiriki: Nawras Mohamed - Msanii, mwanablogi na mshairi, Dr. Hassan Abd Radi – Mkurugenzi wa idhaa ya redio Iraki IMN, Dr Mouna Taleb Al Badry – Mkuu, Kitivo cha Elimu ya Michezo kwa Wasichana, Bw. Abdul Raheem Yassir – mchoraji vibonzo vya kisiasa.

Maelezo Zaidi:  Umoja wa Mataifa nchini Iraki ulipangilia Kipindi cha Moja kwa Moja cha Ulimwenguni kote cha kipekee na jopo ambalo lilijumulisha mseto wa mashirika ya kiserekali, wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya serikali na Umoja wa Mataifa ili kuzungumzia masuala yanayozungukia amani endelevu na namna ambavyo Siku ya Amani inavyoweza kutumiwa kuunganisha watu kote Iraki. Mada ilikuwa Amani na Utamaduni

Ili kutazama filamu inayoainisha msaada wa UNDP nchini Iraki kuhusu Siku ya Amani katika miaka iliyotangulia, bofya hapa.

New York, Marekani

Mwenyekiti Wake: CISV

Maelezo Zaidi: Kwenye Siku ya Amani ilileta pamoja kundi la vijana kwa ajili ya mazungumzo yenye kusisimua kuhusu namna ambavyo vijana wanavyoweza kuimarisha amani kuzidisha ushirikiano wa kati ya tamaduni na kuwa sehemu ya mchakato wa kujenga amani katika jumuia yao. Kwa miaka yote CISV imeweza kuhamasisha wahusika wengine wa kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Amani kupitia katika muziki, densi na kandanda kwa hivyo basi Kipindi hiki cha Moja kwa Moja Ulimwenguni kote kiliweza kuwaunganisha watu binafsi na mashirika ili kuzungumzia namna ambavyo wanavyoweza kukuza ufahamisho katika miaka ijayo.

Ifuatayo ni mifano ya msaada wa CISV katika miaka ya awali.

 

Here are examples of CISV's support in the previous years

San Salvador, El Salvador

Mwenyekiti Wake: Isabel Aguilar Umaña - Interpeace

Washiriki: Raúl Mijango – Mraritibu wa genge la kusitisha vita nchini El Salvador, Monsignor Fabio Colindres – Mratibu wa genge la kusitisha vita nchini El Salvador, Salvador Ruano – Diwani wa  Ilopango, Antonio Cabrales – Rais wa wakfu wa kibinadamu (Fundación Humanitaria).

Maelezo Zaidi: Kipindi cha Moja kwa Moja Ulimwenguni kote kililenga katika kazi ambazo zimefanywa na serikali, mashirika ya vyama vya kiraia na wanachama wa genge ambao walisababisha usitishaji wa vita kati ya magenge mawili pinzani, Mara Salvatrucha 13 (MS-13) na Barrio 18 mnamo mwaka 2012. Jopo lilijumuisha watu binafsi kutoka katika mazingira mseto wa mazingira tofauti ili kuzungumzia namna ambavyo usitishaji vita huu unavyoweza kusaidi katika kujenga amani katika jumuia pana zaidi kwenye Siku ya Amani Septemba 21.

 Ili kupata kujua zaidi kuhusu usitishaji huu wa vita tafadhali bofya hapa

 

Mosko, Urusi

Mwenyekiti Wake: Katerina Gordeeva – Mtangazaji wa TV

Washiriki:Sergei Zheleznyak – Makamu wa Spika  Duma, Serikali ya Urusi, Tatiana Lazareva – Mtangazaji wa TV, Irina Yasina – Mtaalamu wa umma na UchumiElizaveta Glinka aka Doctor Liza – Mkuu wa wakfu ya msaada, Spravedlivaya Pomosh, Dmitry Muratov – Mhariri Mkuu wa Novaya GazetaChulpan Khamatova – Mwigizaji wa Kike, Dr Leonid Roshal – Daktari wa watoto

Maelezo Zaidi: Kufuatia uzinduaji wa kipekee kote nchini Urusi mnamo mwaka 2013 kwa kuunga mkono Siku ya Amani Peace One Day iliwaleta pamoja Wajumbe wa Sirikali, wanachama wakuu wa vyombo vya habari na shirika la sanaa ilikuzungumzia namna ambavyo ujumbe wa Siku ya Amani utakavyoenezwa zaidi kote nchini Urusi. Kwa kufanya hivi waliendeleza ule ufanisi ambao Peace One Day tayari ilikuwa imetekeleza na kuona kote nchini.

Ifuatayo ni misuru ya kauli za uungaji mkono kutoka Urusi

Afghanistan

Maelezo Zaidi: Mikataba ya Siku ya Amani iliyofanywa na wahusika wote waliokatika mgogoro nchini Afghanistan tangu mnamo mwaka 2007 ambao walikubali ule mradi wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza na watoto wapato milioni 4.5 katika sehemu ambazo zilidhaniwa haziwezi kufikika au zilikuwa ngumu kufikiwa kutokana na mgogoro iliwezwa kufanywa.

Kwa Siku ya Amani ya mnamo mwaka 2013, Peace One Day iliweza kuwa mwenyeji wa Kipindi cha Moja kwa moja Ulimwenguni kote kutokea nchini Afghanistan ili kuchunguza namna ambavyo Siku ya Amani inavyowezakuendelea kuimarisha Amani kote nchini. Katika muda huu waliweza kuzingatia katika namna ambavyo vijana wanaweza kufanyakazi kwa pamoja kwa siku zijazo zenye amani zaidi wakianzisha nakufuatiliza utamaduni wa amani na ushirikiano ambao ungekuwa msingi thabiti kwa amani ya kudumu katika nchi hiyo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Mwenyekiti Wake: Balemba Balagizi -  Askari wa Mbugani wa Virunga na Afisa wa Mawasiliano

Washiriki: Ephrem Balole – Mkuu wa Maendeleo ya Mbuga ya Kitaifa ya Virunga, André Bauma – Mkuu wa Hifadhi ya Masoke na Ulinzi wa Wanyamapori, Valérie Katungu Kawa – Mjane wa ranger aliyepigwa risasi mnamo Julai mwaka huu na majangili akichoma makaa haramu, Justine Byandagara – Mwanachama mkuu wa jumuia.

Maelezo Zaidi: Kipindi hiki cha Moja kwa Moja Ulimwenguni kote kilitokana na mbuga ya Kitaifa ya Virunga kwenye mkoa wa Kivu na kikawawaleta pamoja watu binafsi wenye mseto mpana na mashirika ili kuzungumzia namna ambavyo Siku ya Amani inavyoweza kutoa fursa ya kujenga amani kote nchini katika kufuata mada ‘Nani Utakayeridhia Naye Amani?’

Mazungumzo na Mokhtar Lamani

Maelezo Zaidi: Katika Kipindi hiki maalum cha Moja kwa Moja Ulimwenguni kote, Jeremy Gilley, Mwasisi wa Peace One Day, aliweza kuunganika na Mokhtar Lamani, mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Nchi za Kiarabu Mwakilishi Unganishi wa Damaskas nchini Siria kwa njia ya skype ilikuzungumzia masuala muhimu yanayozungukia uwezekano wa amani nchini Siria.