Menu
  • العربية العربية
  • 繁體中文 繁體中文
  • English English
  • Français Français
  • Português Português
  • Русский Русский
  • Español Español
  • Kiswahili Kiswahili

Mnamo Alhamisi Mei 22 katika Salle des Etoiles Peace One Day itaandaa mlo wa usiku wa tamasha nchini Monako. Hafla hii itakuwepo na mnada wa moja kwa moja ukiandaliwa kwa ushirikiano wa Christies na ukisaidiwa kirasmi na Johnnie Walker Blue Label. Bingiriza chini ili kuona maelezo mingine.

Kama huwezi kuhudhuria, lakini ungependa kuchangia katika mnada huo tafadhali bofya kwenye nambari ya simu na fomu ya kushiriki zabuni bila kuwepo zilizo hapa chini.

 

Awamu ya 1: Upande wa Mbele wa Jukwaa la Kumalizia la Lotus F1 Wa Romain Grosjean

Upande wa mbele wa gari hili lililotumiwa na  Romain Grosjean katika kukamilishia jukwaa la Mashindano ya Tuzo Kuu ya Kihindi la mwaka 2013 ni kifaa ambacho kina ushawishi mkubwa zaidi wa taaluma hii kwenye gari la mashindano haya ya Lotus E21 Formula 1. Hii ni sehemu pia ya gari hili ambalo lina nembo ya Peace One Day. Kwa makadirio ya utendakazi na nyenzo zilizotumika, gharama ya kuunda upande huu wa mbele wa gari hili ni Dola $150,000 na hii haijajumulisha usanii wake, ufinyanzi wa CFD na vilevile ule muda wa handaki la kupitisha upepo. 

Mashindano ya Tuzo Kuu ya Kihindi ya mnamo mwaka 2013 yalifanyika mnamo Oktoba 27 na gari hilo aina ya Romain Grosjean lilikamilisha mashindano hayo kwa kasi ya wastani wa 200.667 mph. Sehemu hiyo ya mbele itaandamana na barua ya uidhinishwaji kutoka katika Kundi la Lotus F1 na imesainiwa na Romain Grosjean. 

Makadirio - YURO 5,000 

Awamu ya 2: Mark Dickens - Seti ya Michoro ya Boksi la F1 Toleo la Anasa Isiyo Kikomo

Mark Dickens

Formula One™ Tume ya Utawala ya Toleo la Anasa Isiyo ya Kikomo ya Box Set of Prints

Toleo la 15

Urefu  50 x 50cm 

Misururu Michache ya Toleo Maalum la Mchoro na Mark Dickens kutoka kwenye mchanganyiko wa media 19 za uchoraji iliyoidhinishwa naye Bw. Bernie Ecclestone.  Mark alialikwa katika kila  Mashindano ya Tuzo Kuu katika msimu wa 2011 na akaombwa kuunda kazi ya sanaa ya upakaji rangi kutoka katika kila shindano. Majopo yote yanaonyesha urembo wa kitamaduni na ujenzi usanifu wa kila jiji linaloandaa mashindano haya pamoja na ule upekee wenye nguvu wa mashindano ya Formula 1. 

Zikiwa zimewekwa katika Kisanduku cha Hifadhi ya Makumbusho, michoro mizuri sana ya toleo la kikomo la misururu ya nyumba zote 19 pamoja na michoro miwili ya ziada ya F1™ World #I na F1™ World #II ambazo zote mbili zinafurahisha na huonyesha filamu ya michoro ya picha zote 19 za asili kutoka kwenye Tume ya FOM ya mwaka 2011.  Mchoro wa toleo dogo la F1™ World #II ni wa kipekee katika kundi hili na si la kuuzwa kwa watu binafsi.

Zikiwa zimechapishwa kwenye karatasi ya sanaa safi kabisa na nyeroro ya Somerset misururu hii iliweza kujumuisha vilevile cheti cha uidhinishwaji kilicho na toleo la idadi finyu na waraka uliosainiwa na Bw. Bernie Ecclestone kuhusu mkusanyiko huo. 

Makadirio – YURO 10,000 

Awamu ya 3: John Walker & Sons Signature Blend, Toleo la Vodafone Mclaren Mercedes

John Walker & Sons Signature Blend, Toleo la Vodafone McLaren Mercedes, vyote vimetengenezwa na chupa 25 tu ambazo zinapatikana na, mpaka sasa, zimeuzwa rejareja pekee katika brand’s House mjini Shanghai. 

Zikiwa na bei ya karibu dola $50,000 John Walker & Sons Signature Blend, Toleo la Vodafone  McLaren Mercedes, mseto maalum wa mivinyo nadra iliyoundwa na bingwa wa formula 1 wa mwaka 2009 Jenson Button, na kumbukumbu kwake Johnnie Walker kutokana na ushirikiano wake wa miaka 8 na Vodafone McLaren Mercedes.

Mvinyo Wetu Mkuu ambao umetokana na matunda yaliyookotwa –kwa mkono na mivinyo ya nafaka yenye ubora wa kipekee kutoka kwenye maeneo yale makuu manne ya kutengeneza ya Scotland. Baadhi ya mvinyo huu umekuweko kwa zaidi ya karne mbili, na mbili kati yazo kwa zaidi ya miaka thelathini. Aidha baadhi ni nadra sana, ukitokea kwenye makampuni ya kuutengeneza ambayo tayari yamefungwa. 

Toleo hili finyu limewasilishwa kandokando ya wheel nut halisi inayotumiwa katika magari ya Vodafone McLaren Mercedes kwenye Mashindano ya Tuzo Kuu ya Hungarian ambayo alishida Jenson Button kwenye kuanza kwake kwa 200th – hivyo basi nikikupa umiliki wa kazi  ya kipekee ya kihistoria ya mashindano ya mbio za magari.  Nakala 20 pekee zilizopatikana kwa uuzaji wa binafsi hali ambayo inafanya toleo hili kuwa nadra kabisa kama lile la Jenson Button – moja la pekee.

Makadirio – YURO 30,000 

Awamu ya 4: Gavin Turk - Camouflage Fright Wig Silver and Orange On Taupe

Gavin Turk

Camouflage Fright Wig Silver na Orange on Taupe, 2007
Toleo la 40
Urefu 1000 x 1000mm 

Gavin Turk ni msanii wa kimataifa aliyezaliwa-Uingereza. Ameanzisha mifumo mingi ya vinyago vya kisasa vya Uingereza ambavyo kwa sasa huchukuliwa kuzawadiwa, vikiwemo vinyago vya shaba, sanamu ya nta, ikoni iliyotumiwa tena kihistoria na matumizi ya takataka katika sanaa.

Kazi na vinyago vya Turk vinashughulikia masuala ya uandishi, uhalali na utambulisho. Akiwa amejali  ‘hadithi za imani’ za msanii na ‘uandishi ‘ wa kazi yake, uhusishwaji wa Turk na usasa huu, mjadala wa avant-garde unarudi nyuma na kuanzia katika zile kazi zilizotayari za Marcel Duchamp. Mnamo mwaka 1991, Royal College of Art ilikataa kumpa Turk shahada kwa misingi kwamba onyesho lake la mwisho, Cave, lilikuwa na nafasi ya studio iliyokuwa imepakwa rangi nyeupe ikiwa na bamba ya turathi ya samawati pekee iliyokuwa ikikumbuka uwepo wake ‘Gavin Turk  alifanya kazi hapa 1989–91’. Na moja kwa moja akawa amepata sifa kuu lakini mbaya kupitia katika kazi hii, Turk aliweza kutambulika  na Charles Saatchi na tangu hapo amekuwa akiwakilishwa na hifadhi nyingi kuu za picha ulimwenguni kote. Turk hivi karibuni amepewa idhini ya kuunda vinyago mbalimbali vya umma kikiwemo Nail, kinyago cha mita-12 kinachopatikana One New Change, kando ya Kanisa la St Paul’s Cathedral London.

Makadirio -  YURO 6,500

Awamu ya 5: Kipindi Cha Kuandika Nyimbo na Wayne Hector

Fursa ya Mara moja katika Maisha ya kushinda kutwa nzima kwenye studio na mtungaji nyimbo pamoja na mtayarishi mkuu na maarufu Wayne Hector.

Wayne Hector ni mwandishi wa nyimbo wa Uingereza wa kutuzwa tuzo mbalimbali aliye pia na tuzo za heshima zikiwemo ‘Wimbo bora zaidi wa Uingereza kutoka katika MOBOs na hata BRITs. amefanyakazi kwa ufanisi ulimwenguni kote na wasanii kama vile One Direction, Nicki Minaj, Pussycat Dolls, Britney Spears, The Wanted, Olly Murs, Rascal Flatts, Mika na JLS. Wayne pia anasifiwa na nyimbo saba za bendi ya Westlife ambazo amezindua moja baada ya nyingine zikiwemo 'Flying Without Wings ' na 'World of Our Own'.

Wayne ameandika nyimbo za kimataifa na zinazozinduliwa moja baada ya nyingine zipatazo zaidi ya 30. Je, utunzi wako ndio utakaofuata?

Makadirio - YURO 15,000

Kumbuka: Siku hiyo kwenye studio itapangiliwa kwa muda na wasaa utakao kubaliwa na wahusika wote 

Awamu ya 6: Nancy Fouts - Peacemaker (look but don't touch)

Nancy Fouts
Peacemaker (look but don't touch), 2014 chuma, mbao na miba iliyopakwa rangi
Urefu 35, kimo, 12, upana sm 6

Msanii Nancy Fouts mzaliwa Marekani ameishi na kufanyakazi London kwa zaidi ya miaka 40. kazi zake Fouts hutuma akili za  mtazamaji wake katika safari ya shauku na msisimko. Kujitolea kwake katika masuala ya ajabu na hukimbiza matarajio ya mtu kwenye kichwa chake. Hupatia akili uhuru wa kupumzika mbali na woga na wasiwasi mkuu wa yale mambo yaliyozoeleka, na ulimwengu uliojitenga wa mambo ya kawaida.

Fouts anafuatiliza utamaduni wa yule anayeamini katika uhalisia kwa kuweza  kuoanisha vitu visivyokuwa na uhusiano na kubadilisha maisha ya kila siku kuwa ya kimazingaombwe tu na akiwa amejitangaza kuwa bahili wa vitu,  ‘fikra hunijia kwa kuangalia vitu upya’, anaelezea Fouts. ‘Mimi hujiuliza tu kinaweza kuwa kitu kipi kingine?’ ‘Kinafanana vipi na  kitu kingine?’ Kama kuna mada katika kazi yangu, Ningefafanua mada hiyo kuwa ‘uhuru wa fikra’.

Fouts anaelezea upya muktadha na kuondoa thamani ishara kuu za nyakati zetu; na wakati huohuo anapatia nguvu vilivyosahaulika au vilivyopitwa bila kuonekana.  Fouts anapatia nguvu mpya za kuangalia na kuangalia tena ili kujifunza na kujifunza tena. Hii ni sanaa hakika ambayo anatumia, Fouts anafikiria kiasi cha kupatwa na ukatili kuhusu kumbukumbu za kihistoria,  imani mafundisho ya kidini  na uhalisia. Nancy Fouts mtu wa nje wa kweli, mtafutaji ‘anayefanana na magpie’ ambaye anachimba migodi ya historia. Kwa kuweza kupindua ishara na ikoni, Fouts anaunda lugha nzuri ya kupendeza na isiyotambulika, ambayo inachanganya na kustaaajabisha mantiki yetu ya ufasiri. 

Nancy Fouts ameshiriki katika maonyesho kwenye hifadhi za picha na hata makumbusho ulimwenguni kote huku mifano ya kazi ya msanii huyu ikipatikana katika nyumba za kibinafsi na mikusanyiko iliyotambulika ulimwenguni kote, ikiwemo ya makumbusho ya Victoria & Albert Museum Jijini London.

Makadirio  - YURO 7,500 

Awamu ya 7: The Connor Brothers - A load of fuss about fuck all (red)

The Connor Brothers
A load of fuss about fuck all ( red ), 2014

Akriliki katika turubai
183 x 124 cm

Akitumia kolagi ili kuficha maana ya kazi mama za kitambo zilizopakwa rangi na riwaya za kimahaba za mvinyo, Connor Brothers waliweza kuonyesha jicho la kuona atakalo tu na pevu katika utamaduni wa kisasa. Kazi zao zinafasiri upya vitu kutoka kwenye historia na kwa kufanya hivyo zinapatia  mazingira ya kisasa mzaha wa kuzungumziwa  haswa yale yaliyo na shauku ya utajiri, umaarufu na dhana isiyokuwa ya kihalisia ya kutangaza maono ya uhusiano. Kazi za Connor Brothers zinaweza kupatikana katika mikusanyiko mbalimbali Ulimwenguni kote ikiwemo ile ya Makumbusho ya Victoria & Albert Jijini London.

Makadirio – YURO 9,500 

Awamu ya 8: Hali ya Lotus F1 iRace

Fursa isiyosahaulika kuweza kupitia na kuona nguvu, maonyesho na teknolojia ya gari halisi la Formula One (F1) awamu hii inawapatia watu wawili fursa ya kuwa dereva wa F1 wa siku hiyo kwenye programu ya mashindano ya kundi la Lotus F1 katika eneo la Paul Ricard (Kusini mwa Ufaransa). Baada ya baadhi ya mafunzo ya muda mfupi kwa kukutayarisha kwa siku yako, utapata fursa ya kuzoena na ule mzunguko wa gari la mashindano ya mtu mmoja, ukiendesha gari aina ya Formula Renault 2.0 kwenye vipindi viwili vya dakika ishirini.

Basi ni wakati wa kitu halisia – kuendesha gari la kusisimua la 700bhp F1 –kilele cha hali ya kuendesha gari. Hatimaye kukupatia msisimko kamili wa gari aina ya F1 katika kasi ya juu, wageni wataendeshwa kwenye mzunguko katika gari la abiria na dereva wa akiba wa Kundi la Lotus F1

Makadirio – YURO 8,000