Menu
Mtandao wa Shule

Nani Utaridhia Kufanya Naye Amani?

Peace One Day inahimiza shule yako au kundi la vijana kujiunga katika Mtandao wa Shule na kuahidi kujitolea kwenu katika Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21. Mtandao wa Shule ni mseto wa Ulimwenguni kote wa taasisi za kielimu na walimu wanaojitokeza kuchukua hatua katika Siku ya Amani mnano Septemba 21.

Ingawaje Mtandao huu ulizinduliwa tu mnamo juni 21 mwaka 2012, Mtandao wa Shule umekua kwa haraka. Mamia ya shule na taasisi za kielimu duniani kote tayari zilikua zimejiunga kufikia Siku ya Amani ya mnamo mwaka wa 2012. Tusaidie kujenga hata mseto mkubwa zaidi wa shule kufikia mnamo mwaka wa 2014. Shule au shirika lako litaweza kuangaziwa kwenye tovuti ya Peace One Day na unaweza kuchagua kupokea habari za hivi punde za mara kwa mara kwenye baruapepe.

Maoni kutoka kwa shule mbalimbali duniani kote kabla na hata baada ya Siku ya Amani ni muhimu sana katika kusaidia Peace One Day kupima athari ambayo shule na vijana wanaweza kusababisha kwenye siku hiyo. 

Kuadhimisha Siku ya Amani Katika Darasa Lako

Kwa miaka yote maelfu ya shule duniani kote yamefikiria kuhusu njia za kufurahisha na gunduzi za kusherehekea Siku ya Amani. Kuanzia katika kuandaa hafla ya michezo hadi kuandika wimbo wa amani  shughuli zinawaza kuwa kubwa, ndogo, za sauti kubwa au tulivu chochote kile ambacho kinawezekana katika shule yako au kundi lako la vijana.

Idara ya Elimu ya Peace One Day inafuraha kuwasilisha mwongozo huu wa shughuli za Siku ya Amani ili kusaidia shule yako kupangilia sherehe yake ya Siku ya Amani. Mwongozo huu wa manufaa unakusanya:

  • Jedwali: kabla, wakati wa na baada ya Siku ya Amani
  • Nyenzo: nembo, mabango na filamu za Peace One Day 

Hoja za ziada za kutilia maanani 

Tunatumai nyenzo zilizotolewa hapa zitakuwezesha wewe na wanafunzi wako kusherehekea Siku ya Amani kwa njia ya kufurahisha, bunifu na yenye maana kubwa.

Fikra za kuadhimisha siku hio:

Vipaumbele vya Siku ya Amani ya mwaka 2012 kutoka kwenye Mtandao wa Shule
Mradi wa Amani ya Kimataifa wa Quilt
Mahali: Dunia nzima

Tangu mwaka 2010 mradi wa Amani wa Quilt umekuwa ukiwaalika vijana kutoka kote ulimwenguni kuweza kuwasilisha mchoro unaoonyesha amani inamaanisha nini kwao. Picha hii baadaye huamishwa kwenye uelewa ulio na vipengele maalum vya usanifu ambavyo vimechaguliwa kwa ufarishi kabla ya kuunganisha picha za shule nyingine ili kuunda Mfarishi wa Kimataifa wa Amani. Wazo hapa nikuweza kuunganisha shule za dunia nzima katika amani, na, mnamo Agosti mwaka 2012, mataifa 200 yaliwakilishwa kwenye mfarishi. Peace One Day ina fahari kushirikiana na shirika ambalo maadili yake yanafanana na yatu.

Tazama filamu ya Peace Quilt ili kujifunza zaidi kuhusu historia ya mradi huu na bofya hapa ili kuona ni lini ambapo Quilt ya Amani itakuwa ikija katika ifadhi ya  picha ilio karibu nawe