Menu

Kama kandanda ni sehemu ya maisha yako na una shauku katika kuitia moyo jumuia iliyo karibu nawe katika masuala ya Amani, basi tafadhali jihusishe na Siku Moja Lengo Moja. Mojawapo ya njia rahisi na ya kufurahisha zaidi ya kuadhimisha Siku ya Amani ni kupangilia mechi ya Siku Moja Lengo Moja (au hata kinyang’anyiro!’)

Kuanzia katika mechi zinazounganisha polisi na wakazi wa nchini Brazil hadi kwenye kiliniki za kandanda kwa ajili ya watoto waliohamishwa nchini Ufilipino, Siku Moja Lengo Moja inaonyesha waziwazi nguvu za kandanda katika kuunganisha watu, kuwapatia tumaini na nguvu za kuimarisha jitihada za ujengaji – amani.

Siku Moja Lengo Moja: Chukua Hatua

Zifuatazo ni baadhi ya rasilimali za kukusaidia kupangilia mechi yako ya Siku Moja Lengo Moja. Kuanzia kwenye vipeperushi na mabango ya Namna Ya Kuongoza, kuna mawazo chungu nzima ya namna unavyoweza kuimarisha ufahamisho wa Siku ya Amani ya mnamo tarehe Septemba 21.

Ili kutuambia kuhusu hafla yako ya Siku Moja Goli Moja tafadhali tuma baruapepe: onedayonegoal@peaceoneday.org na uongeze mechi yako ya kandanda katika mechi ya maelfu ya wengine wanaocheza kwa kusudio la amani.  

Siku Moja Lengo Moja Katika Mashule.

Idara ya Elimu ya Peace One Day huleta amani kwenye madarasa kupitia kwenye rasilimali za Elimu za bila malipo.

Huu ni mpango wa kipindi unaowaomba vijana kuweza kuchunguza nguvu za michezo katika kuleta watu pamoja, ikiwemo mechi ya kandanda inayochezwa katika ardhi ‘isiyo milikiwa na yeyote’ kwenye msimu wa Krisimasi katika Vita ya Kwanza ya Dunia.

Coaches Across Continents

Huu ni ukurasa uliotengwa tu kwa ajili ya Siku Moja Lengo Moja na timu ya kipekee ya Makocha kwenye Mabara Yote Ulimwenguni ambao wameunda misururu ya michezo itakayokusaidia kuweka pamoja mbinu za kusuluhisha mgogoro katika utoaji mafunzo yako ya kila siku ya kandanda.

Ujumbe wa Msaada

Siku Moja Lengo Moja inaungwa mkono na mamia ya mashirika Ulimwenguni kote. Kutana na aliyekuwa mshambuliaji wa Uingereza na bigwa maarufu wakichangia sauti zao katika uanzilishi huu.

Eric Murangwa Eugene

Jifunze vipi ambavyo kandanda iliyaokoa maisha ya Eric Murangwa Eugene kwenye mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mnamo mwaka 1994. 

Hadithi za Siku Moja Lengo Moja

Mnamo mwaka 2014 zaidi ya watu 35,000 waliweza kucheza zaidi ya mechi 2,100 za Siku Moja Goli Moja katika nchi 193. Angalia albamu yetu ya Facebook ili kutazama namna ambavyo wabia wetu wanatumia kandanda katika kusherehekea Siku ya Amani, September 21.

Rwanda

Kandanda kwa Tumaini, Amani na Umoja (FHPU) iliweza kuandaa shughuli za Siku Moja Goli Moja mjini AMAHORO katika sehemu kumi kote nchini Rwanda pamoja na kuandaa mechi mjini London, Uingereza ili kusherehekea Siku ya Amani ya mnamo 2014 na kuimarisha urafiki baina ya vijana kote nchini. Zaidi ya washiriki 1500, walio na umri kati ya 7-35, waliungana pamoja kutoka kwenye mikoa mitatu, ikiwemo mara ya kwanza, timu ya Kikongo kutoka Goma (wilaya ya Rusizi), ili kucheza mechi zilizoundwa kwa nia ya kuhimiza uimarishwaji wa amani kati ya mipaka. 

Rio de Janeiro, Brazil

Siku ya Amani ya mnamo 2014 iliweza kusherehekewa na NBS Rio+Rio kwenye nyumba za vibanda za mji mkuu, jumuia husika zilipewa moyo kutokana na Kombe la Dunia la Kandanda la FIFA 2014 lililofanyiwa uko hivi majuzi. Mechi hizo zilichezewa Inferno Verde (Green Hell) sehemu iliyo ndani ya Complexo do Alemão ambayo ni maarufu ulimwenguni kote kama mojawapo ya sehemu ya nyumba za vibanda hatari zaidi. Uwanja huu ulikuwa kwenye barabara ya Itararé, inayojulikana kama Gaza Strip, sehemu ambayo iliogopewa lakini kwa siku moja iligeuzwa na kuwa mahali pa michezo pale ambapo jumuia za eneo ilo ziliungana pamoja kusherehekea siku ya amani na kuweza kuwapatia vijana wa hapo fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika kandanda. 

Monrovia, Liberia

Kandanda ili Kuendeleza Umaskini (FODEDE) iliweza kutumia hafla ya Siku Moja Goli Moja ili kukuza ufahamu sio tu wa Siku ya Amani lakini pia kuhusu Virusi vya Ebola. Programu yao ya Siku ya Amani ya mnamo mwaka 2014 kwa jina “Kukomesha Ebola nchini Liberia” ilijumuisha gwaride kupitia katika jumuia ya hapo, michezo ya kandanda na mchezo wa kickball, mchezo aina ya kandanda ya kitamaduni unaochezwa na wanawake nchini Liberia.

Uvira, DRC

Centre des Jeunes pour la Paix iliweza kupangilia siku yenye shughuli na mechi ya kandanda kwa ajili ya Siku ya Amani ya mnamo 2014. Mechi hizi ziliweza kuwaleta pamoja vijana kutoka kwenye jumuia yote ambazo awali ziligawanywa na mgogoro. Kundi hili lilitumia hafla yao ya Siku Moja Goli Moja katika kutekeleza mipango ya mafunzo ya Makocha kwenye Mabarani Yote (CAC) kuhusiana na mawasiliano, usuluhishaji wa mgogoro na usawa wa jinsia. Zilihamasisha timu za kandanda zenye mseto wa jinsia ili kukabiliana na kauli mbalimbali kuhusu jinsia na kuweza kuweka wazi majadiliano yanayohusu wajibu wa jinsia miongoni mwa vijana. 

Jiji la Zamboanga, Ufilipino

Mnamo 2014 - Philippine Marine Corps (PMC) iliweza kuandaa mechi za kandanda zipatazo 170 za Siku Moja Goli Moja kwenye jiji la Zamboanga kwenye kisiwa cha Mindanao kama ishara ya maendeleo kutoka mnamo mwaka 2013. PMC iliweza pia kuimarisha Manila & Tawi-Tawi hadi kiwango kikubwa, na kuleta pamoja jumuia mbalimbali kwa ajili ya amani.

Mnamo mwaka 2013 – Oktoba 4, PMC iliandaa hafla ya kandanda ya Siku Moja Goli Moja kwenye eneo lililoathirika na vita ya Zamboanga. Hafla hii iliandaliwa baada ya kuahirishwa kutoka kwenye mipango asilia ya Siku ya Amani kutokana na hali ya vurugu katika jiji hilo. Hafla hii iliweza kutoa mazingira salama kwa vijana walioathirika na mgogoro huu na kuwaunganisha ili kucheza kandanda na kukumbuka namna ilivyo kuwa kijana.

 

Rio de Janeiro, Brazil

Afisa wa polisi kutoka kwenye Kitengo cha Polisi cha Amani (UPP) na wakazi wa jumuia wa Morro da Mangueira, ‘walizozana’ katika Siku ya Amani

Kwa wengi, hiki ni kichwa cha habari maarufu sana katika magazeti ya huko, hata hivyo wakati huu mzozo ulikuwa tofauti kwani ulipelekwa hadi uwanja wa kandanda katika sherehe ya Siku ya Amani, mnamo tarehe Septemba 21. Kwa hivyo nani aliyeshinda mechi hiyo? Kila mtu. Kwa sababu kwa kuweza kucheza mtu kando ya mwengine, wakazi na wa UPP wa RIO waliweza kuonyesha kwamba wanaweza kuungana pamoja ili kuunda amani katika jumuia yao.

CISV Ekwado

CISV Ekwado iliadhimisha Siku ya Amani katika kinyang’anyiro cha kipekee kilichowaleta vijana pamoja kupitia kandanda kwenye Siku ya Amani.

Port-au-Prince, Haiti

Maelfu ya watazamaji walikuja pamoja kuwa sehemu ya kinyang’anyiro cha Siku Moja Lengo Moja kilichofanyika katika uwanja wa kitaifa katika hali ya kusherehekea Siku ya Amani na wakaweza kuwatia moyo wengine kwa kuwapa tumaini pamoja na umoja katika nchi ambayo bado inajikokota kutokana na athari kubwa ya kutisha ya mtetemeko wa ardhi uliofanyika mnamo Januari mwaka 2010.

Imeandaliwa na Idara ya Elimu ya Maendeleo ya Vijana ya Haiti (Haiti Youth Development Education (H.Y.D.E.)) 

Khanaqin, Iraki

Jeshi la Iraki na Kurdish Peshmerga – majeshi mawili ambayo kwa kawaida hupigana na kuzozana baina yao yaliweza kuja pamoja mnamo mwaka 2008 na kuweza kucheza mechi ya kirafiki na kusherehekea ODOG. Mercy Corps aliweza kufanya kazi kwa karibu na Peace One Day katika kuzileta pande hizi pamoja na kuwezesha kusherehekea amani kupitia kandanda.

Imeandaliwa na Mercy Corps

Rio de Janeiro, Brazil

Mechi ya Umoja iliweza kuchezwa kati ya watoto kutoka kwenye ujirani wa favelas (miji duni) mjini Rio. Favelas ni sehemu ambayo hivi karibuni imeweza ‘kukumbatia’ amani, kumaanisha kuwa sehemu hii haiendeshwi tena na magenge yanayoandamana. Kuandaa mechi katika uwanja huo ilikuwa ishara kuwa walikuwa wamekuja pamoja katika sehemu ambayo ilikuwa inaendeleza vurugu ya magenge hayo, hafla hii iliweza kuwapatia wakazi fursa ya kipekee kutoka katika favelas tofauti na kutangamana na kuzungumza – jambo ambalo hawakuweza kufanya hadi hivi karibuni.

Pyongyang, Korea Kaskazini

Timu ya Wanawake ya Kandanda ya Middlesbrough FC ilisafiri hadi Korea Kaskazini kucheza mechi 2 dhidi ya timu za huko, kwa kuweza kuunga mkono Peace One Day. Hafla hii ilikuwa ni hali ya kustastajabisha kwa wale waliohusika, iliendeleza ushirikiano kati ya tamaduni na kusherehekea kumbukumbu ya miaka 10 ya uhusiano wa miaka ya kidiplomasia ya Uingereza na DRPK.

Imeandaliwa na Koryo Tours