Menu
Je, Nani Utadensi Naye?

Kama wewe ni mwanadensi, mwalimu wa densi au kwa ufupi mtu anayependa kucheza densi, basi Siku Moja Densi Moja ndiyo njia bora zaidi ya kuonyesha shauku yako ya amani katika Siku ya Amani ya Septemba 21. Ama wewe ni mwelekezi wa densi, unajitolea katika kipindi chako au unapangilia mikusanyiko ya watu – Siku Moja Densi Moja iko wazi kwa ufasiri wako wa ubunifu.

Tueleze kuhusu mipango yako ya Siku Moja Densi Moja na fikra zako tafadhali tuma baruapepe: dance@peaceoneday.org na uongeze densi yako katika densi za watu maelfu wanaocheza kwa Amani.

Jinsi Gani Kucheza Densi Kunaweza Kuwapa Moyo Watu Kuwa na Amani?

Siku Moja Densi Moja imeweza kushuhudia maelfu ya watu kutoka ulimwenguni kote wakicheza kwenye Siku ya Amani, mnamo Septemba 21. Kutoka kwenye makundi makubwa ya wachezaji densi nchini Lithuana na Visiwa vya Cayman, hadi katika maonyesho ya shule nchini Urusi na Kenya, mnamo mwaka 2014 watu wa kujitolea na wataalamu waliungana pamoja ili kutetea amani, wakiwa na zaidi ya densi 760 katika nchi 66.

Albamu ya Facebook ya Siku Moja Densi Moja

 

Hadithi za Siku Moja Densi Moja
Vipaumbele vya 2014

Kundi kubwa la wacheza densi la International Zouk Flashmob

Tangu mnamo mwaka 2012, kundi kubwa la wacheza densi la International Zouk Flashmob (IZFM) katika uanzilishi wao wa kila mwaka limekuwa likilenga katika kuunganisha ulimwengu kupitia katika densi maarufu kutokea Brazil iitwayo Zouk. Mnamo mwaka 2014, takribani wachezaji densi 4000 kutoka katika miji 162 katika nchi 34 walicheza kwa mtindo sawa wa Zouk kwa ajili ya amani ulimwenguni kwenye Siku ya Amani. Mnamo mwaka 2015, IZFM itaweza tena kufanyika mnamo September 21. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea www.ZoukInternational.com

Speak Out Uganda

Mradi wa Ongea katika eneo la Katanga uliweza kuandaa sherehe za Siku ya Amani zilizojaa furaha na uchukuaji hatua, zilizojumuisha densi, mashindano ya muziki wa kufoka na onyesho la kuendesha baiskeli kwenye uchafu.

Tafrija ya Siku ya Amani Sydney, Australia

Tafrija ya Siku ya Amani Sydney ilikuwa yenye ufanisi wa kipekee kwa mara nyingine mwaka huu, ikiwa na zaidi ya watu 700 waliofurahia mseto mpana wa maonyesho. Hii hapa ni picha ya ‘Malaika wa Amani’ wakiwa jukwaani.

God in Us Africa, Rwanda

God in Us Africa, iliweza kutumia densi kama mbinu ya kuwafunza watoto wa eneo hilo katika mji wa Gisenyi kuhusu dhana za amani, heshima, maridhiano, kusameheana, tumaini na uvumilivu.

Vipaumbele Vya 2013

Mkusanyiko wa Watu wa Zouk Kimataifa (International Zouk Flashmob IZFM)

Kila mwaka Mkusanyiko wa Watu wa Zouk wa kimataifa (IZFM) huimarisha aina moja ya katika makundi ya Zouk duniani kote ili kuweza kukuza ufahamisho wa Siku ya Amani ya Septemba 21. Katika IZFM ya mwaka 2013, takribani wanadensi 3500 kutoka miji 127 katika nchi 43 waliungana pamoja ili kucheza Densi ya kutoka Brazil iitwayo Zouk kwa ajili ya amani na upendo wa ulimwengu. Ili kujihusisha katika densi ya mwaka huu. Tafadhali angalia katika ukurasa wao.

Eneo la Mkusanyiko wa Watu la Trafalgar Square 

Tom Morley na Silaha za Muungan0isho wa Wengi (Weapons of Mass Connection) waliweza kuwaweka pamoja Mkutano la Amani la JCI London (JCI London Peace Conference) na Wapiga Ngoma (Pandemonium Drummers) wakubwa katika kuwasilisha mikusanyiko ya watu ya kipekee kwenye eneo maalum liitwalo Trafalgar Square, London ili kusherehekea Siku ya Amani ya mnamo mwaka 2013.

Kundi la Wonyeshaji Sanaa la Amrita (Amrita Performing Arts)

Ikiwa ni Sehemu ya Siku Moja Densi Moja, wanadensi wawili kutoka kwenye kundi la Waonyeshaji Sanaa wa Amrita (Amrita Performing Arts danced in Phnom Penh, Cambodia on top of the iconic White Building to celebrate peace on 21 September.  

Siku Moja Densi Moja: Chukua Hatua

Zifuatazo ni baadhi ya rasilimali za kusaidia kuadhimisha Siku ya Amani ya mnamo tarehe Septemba 21 kupitia katika matukio ya densi.

Kwa ajili ya rasilimali nyingine tembelea ukurasa wetu wa Rasilimali.