Menu
Kitabu cha Amani cha Mfukoni (The Pocket Book of Peace)

Huwa si mapema kuanza kupanga kile utafanya ili kuadhimisha siku. Bofya hapa ili kupata Kitabu cha Amani cha Mfukoni ambacho kitakupa mawazo na rasilimali itakayokusaidia kuadhimisha siku hii

Unaweza kupangilia shughuli mwaka mzima ambazo zitatusaidia kuangazia ufahamisho wa Siku ya Amani ya Septemba 21 na kuhimiza wengine kujiunga kwenye kampeni ya 2014.

Hata hivyo ukichagua kuadhimisha, haijalishi kiwango cha shughuli utakachofanya, kujitolea kwako ni muhimu. Ni kushiriki kwa watu wengi kutoka kote ulimwenguni ambako kutaleta nguvu zinazohitajika kuzipa moyo serikali ili kufuata nyayo. Ni juhudi zetu kwa pamoja ambazo zitachangia kufaulu kwa Siku ya Amani ya 2014.

Kurasmisha Siku ya Amani kutakuwa maono ya kila mmoja.

Miongozo

Bofya hapa chini kwa miongozo ya namna ya kutumia rasilimali kwenye ukurasa huu na vilevile maelezo kuhusu kuchanga na kupangilia hafla.

Mtandaoni

Mabango na Rasilimali za Sanifu Mtandaoni

Ifuatayo ni miseto ya mabango mbalimbali ya Peace One Day ambayo unawza kutumia katika blogi, tovuti na majukwaa ya mitandao ya kijamii ili kuonyesha msaada wako kwenye Peace One Day na kueneza ufahamisho kupitia katika mtandaoni.

Vipimo vinatolewa, lakini kama utahitaji ukubwa tofauti, tafadhali wasiliana na Kundi la Wanahabari wa Mtandao wa Kijamii wa Peace One Day.

Misimbo ya QR

Huu hapa ndio msimbo wa QR ambao unaelekeza watu kwenye www.peaceoneday.org ambapo watapata kujihusisha. Unaweza kupachikwa kwenye mabango, vipeperushi na majukwaa ya kidijitali.

Arifa za Mtandaoni

Hili hapa ni chaguo la matangazo ya mtandaoni ambayo yamejitolea kwa mada ya kampeni ya Peace One Day: Nani Utaridhiana Naye Amani? Ambayo yanaweza kupakiwa kwenye majukwaa mtandaoni, ikiwemo, blogi na majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Misimbo Pachikwa ya Video

Ili kuufahamisha mtandao wako wa mtandaoni na kukuza ufahamisho wa Peace One Day tafadhali kuwa huru kupachika video za YouTube videos za filamu muhimu za Peace One Day kwenye tovuti yako, blogi au umbo lako la mtandao wa kijamii.

Violezo vya Vyombo vya habari vya Kijamii

Bila shaka kuwa huru kuimarisha Peace One Day kwa njia yoyote ile ungependa lakiki ukitaka kusaidia tafadhali pata violezo vya vyombo vya habari vya kijamii vikiwa na viungo muhimu ambavyo vitagawizwa kote katika mitandao mikuu ya kijamii ikijumuisha Facebook, Google+ na Twitter.

Nembo za Peace One Day

Hii hapa ni nembo ya ‘Kwa msaada wa’ ili kuonyesha msaada wako katika Peace One Day.

Tafadhali usibadilishe nembo hii.

Umbizo la JPG 

Kuunga mkono Shughuli zako za Siku ya Amani

Kiolezo cha Waandishi wa Habari

Ufahamisho wa Siku ya Amani huunda hatua, na hatua hiyo huokoa maisha. Kuangazia ufahamisho wa shughuli zako za Siku ya Amani kupitia vyombo vya habari itaunga mkono lengo letu la kurasmisha siku hiyo, kuifanya iwe endelevu yenyewe.

Kama inawezekana, alika vyombo vya habari katika hafla yako (Televisheni, redio, magazeti na majarida). Ili kukusaidia na haya, hapa kuna kiolezo cha habari kwa wanahabari. Kuwa huru kuongezea maelezo zaidi ambayo yatawakilisha shughuli zako vizuri.

Vipeperushi

Tumeunda mseto wa vipeperushi kukusaidia kukuza ufahamisho wa Siku ya Amani.

Utambulisho wa Peace One Day