Menu

Kampeni mpya ya kusisimua ya mwaka 2015 kwa kutumia ragbi katika kuhamasisha watu kuhusu Siku ya Amani, Septemba 21

Mchezo siku zote umekuwa sehemu kuu ya kusherehekea Siku ya Amani, kuhamasisha watu kuhusu siku hii na kuunganisha watu kwa njia nzuri. Mchezo hufunza ushirikiano, huimarisha mazungumzo, hupunguza kutoelewana na ni kiungo muhimu sana cha kuimarisha amani na maendeleo. Kwa mfano, kampeni ya Siku Moja Goli Moja imeshuhudia mechi za kandanda nyingi zikichezwa katika kila taifa mwanachama wa UN kwa ajili ya amani.

Peace One Day imezindua Jaribu kwa ajili ya Amani, uanzilishi ambao utatumia ragbi katika kuwaleta watu pamoja mnamo Septemba 21. Iwe unacheza mchezo wa kitaalam au unacheza tu na rafiki zako fanya hivyo kwa amani.

 

Kwa Nini Ragbi?

Kumekuwa na mifano isiyohesabika ya mchezo huu wa ragbi kuunganisha tofauti mbalimbali na kuwaleta watu pamoja. Mnamo mwaka 1995 Nelson Mandela alivaa jezi ya Francois Pienaar wa Springbok kwenye Kombe la Dunia la mchezo wa ragbi na hivyo basi kuunganisha taifa hilo lililokuwa limegawanyika ili kushabikia timu moja. Mnamo mwaka 2013, ubingwa wa ragbi wa kihindi wa walio na umri wa chini ya miaka 19 uliweza kuandaa mchezo kati ya India na Pakistan, mchezo ambao ulifanya migawanyiko na wasiwasi wote kati ya nchi hizi mbili kutoweka kwa kipindi cha dakika 80.

Hadithi hizi za kusisimua zinaonyesha wajibu wa ragbi katika kuimarisha ulimwengu wenye amani zaidi, hivyo basi kwa Siku ya Amani, kama una shauku kuhusu ragbi na uhimarishwaji wa tabia ya amani, kwa nini usicheze kwa ajili ya amani kama sehemu ya Jaribu kwa ajili ya Amani?

Namna ya Kushiriki

Kunazo njia nyingi za kujihusisha:

  1. Andaa mechi ya #TryforPeace: Uwe ni sehemu ya timu au unafurahia tu kucheza ragbi, kwa nini usiandae mechi au kiny’ang’anyiro kwenye au kabla ya Siku hiyo ya Amani. Usisahau kuwa kama tayari unacheza mechi, kwa nini usijitolee kuiweka mechi hiyo kuchezwa kwenye Siku ya Amani! 
  2. Sajili shughuli zako za Jaribu kwa ajili ya Amani: kutufahamisha kuhusu shughuli zako za Siku ya Amani kwa kuzisajili hapa. Hii itatusaidia kupima athari ya Siku ya Amani na kwa kuwapatia motisha wengine kuweza kushiriki.
  3. Kuja ujumuike pamoja ili kutazama mechi hiyo: Mechi zako zitasaidia kuwaleta watu pamoja kupitia kwa mchezo. Kutokana na mechi yako kwa nini usipige picha za timu hizi zikiwa pamoja na zikisalimiana. Picha hizi zinaweza kuwekwa kwenye mtandao wa kijamii kwa kutumia anwani #TryforPeace na #PeaceDay au kututumia baruapepe kwa tryforpeace@peaceoneday.org
  4. Tuma ujumbe: Kama utaweza kuandaa mechi kwa nini usitume ujumbe kwenye majukwaa yako ya mtandaoni ukilijibu swali hili: Utaridhiana Na Nani Kwa Amani?