Menu
Idara ya Elimu ya Peace One Day: Habari na Matukio...

Machi 19, 2013

Aprili 5, 2013 Aprili 24, 2013

Friend Our World (Rafiki wa Dunia Yetu)

Rafiki wa Dunia Yetu inaundwa na Skoolbo kwa kushirikiana na Peace One Day na Microsoft. Rafiki wa Dunia Yetu ni kitovu cha kujifunza mtandaoni kwa watoto ambacho kinalenga kuwaunganisha kwa pamoja kwa michezo ya kirafiki kuhusu jiografia, lugha na uraia wa ulimwenguni kote. Kitengo hiki kitaenda mtandaoni moja kwa moja mnamo Septemba 2013.

PeaceTalk 3

Jeremy alisafiri na ndege hadi Rio de Janeiro, Brazil ili kuweza kuratibu Mazungumzo ya Amani kati ya Escola Dinamis mjini Rio na Shule ya Upili ya Burlington mjini Massachusetts, Marekani. 

PeaceTalk 4

Jeremy alisafiri na ndege hadi Medellín, Kolombia ili kuratibu Mazungumzo ya Amani ya nne kati ya shule ya Kolumbas mjini Medellin na Shule ya Msinngi ya McWhorter , Texas, Marekani

     
Kwa habari za hivi punde:
Jiandikishe kwenye ukurasan wetu wa Facebook page
Jiandikishe kwenye habari zetu za Twitter feed

 

Ushirika Wa Elimu wa Peace One Day

Kongamano la Elimu la Kimataifa

Bofya hapa ili kutazama wasilisho kuu la Jeremy la mnamo tarehe 14 bila malipo, mtandaoni, Kongamano la Elimu la Kimataifa. la kujumuika la mnamo mwaka wa 2012. Linalofanywa kila mwaka na kuendelea kwa masaa 24 kila siku kwa siku tano mfululizo kwenye Wiki ya Kimataifa ya Elimu (mnamo Novemba 12-17 mwaka 2012), Kongamano hili ni shirikishi, ni uanzilishi wa jumuia ya ulimwenguni kote inayohusu wanafunzi, waelimishaji na mashirika katika viwango vyote. Limeundwa kuweza kuongeza pakubwa fursa za kujenga miunganisho inayohusiana na elimu ulimwenguni kote huku pia ikiunga mkono ufahamisho wa kitamaduni na utambuzi wa mseto uliopo kati yetu. Unaweza kutazama rekodi za wasilisho hili kutoka kwenye kongamano la mnamo mwaka 2012 hapa. Shukrani kubwa iwaendee Wenyekiti Wenza wa kongamano Lucy na Steve kwa kualika Peace One Day kushiriki.

 

 

Mjadala Kuhusu Kuharakisha Elimu

Tembelea ukurasa wa Storify Ili kupata maoni bora zaidi kutoka kwenye mtandao wa kijamii yaliyotolewa kwenye Mjadala wa Kuharakisha Elimu wa mnamo Julai 10 mwaka 2012. Jeremy aliweza kutoa hotuba kuu kwenye mjadala huo, uliokuwa na mada 'Kutoa kwenye Sauti ya mwanafunzi hadi Amani ya Ulimwenguni kote’, mada ambayo ni kiini cha kampeni za idara ya elimu ya peace one day. Alizungumzia kuhusu nguvu za kuhusisha vijana, Jeremy aliweza kuangazia umuhimu mkuu wa Sauti ya Mwanafunzi katika kujenga ulimwengu ulio na amani zaidi. Wanafunzi katika nchi 14 katika mabara yote 6 walichangia katika mazungumzo hayo ya masaa mawili kupitia kwenye kiungo cha video. Vilevile mwengine aliyekuwa akiongea ni mwasisi wa TakingItGlobal, Michael Furdyk, na aliyekuwa mtoto askari nchini Sierra Leonean Mohamed Sidibay. Tungependa kushukuru Promethean Planet kwa kuwa mwenyeji wetu katika hafla hii ya kipekee. Tafadhali bofya hapa ili kutazama vipaumbele vya video.