Menu

Rwanda: Katika Mtazamo

Idadi ya watu mnamo mwaka wa 2011 (ilikadiriwa, 000)  - 10,943

Eneo - 26,338 sq km

Uwezekano wa uhai katika wakati wa kuzaliwa (wanawake na wanaume, miaka) 57.1 / 54.5

Jumla ya Mapato ya Kila Mwaka (US$)* - Dola Bilioni 7.103 Billion

Mpangilio wa Kiolezo Cha Maendeleo ya Kibinadamu ** - 167 (kati ya 186)

 

Chanzo: UN Data, *World Bank & **UNDP

Mseto wa Wanachama wa Peace One Day Nchini Rwanda

Mseto wa Shirika Lisilokuwa la Kiserikali

Mseto wa Wanafunzi

Uzinduliwaji wa Siku ya Amani 2013

Football for Hope, Peace & Unity - FHPU (Kandanda kwa Tumaini , Amani na Umoja)

Siku Moja Lengo Moja

FHPU ilianzishwa mnamo mwaka 2010 na inalenga katika kutumia kandanda kuwa zana ya kuimarisha umoja na maridhiano miongoni mwa vijana wa Kinyarwanda ili kuzuia majanga kama vile mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mnamo mwaka 1994. Pamoja na haya FHPU husaidia pia maendeleo ya kibinafsi ya vijana wanaocheza kandanda kwa kusudio kubwa zaidi na hali kubwa zaidi ya nafsi zao.

Ili kuadhimisha Siku ya Amani 2013, FHPU iliweza kuandaa zaidi ya  mechi 80 za Siku Moja Lengo Moja, ikiwa na wachezaji 1500 katika sehemu saba tofauti nchini Rwanda, pamoja na jumuia za Afrika Mashariki mjini London.  

Ili kupata kujua zaidi kuhusu kazi ya FHPU hapa.

Ili kutazama filamu ya mwasisi wa FHPU, Eric Murangwa Eugene bofya hapa

 


Institute of Research and Dialogue for Peace (Tasisi Ya Uchunguzi Na Mazungumzo Kuhusu Amani)

Shirika mwenzi la Interpeace

IRDP inachangia katika ujengaji wa amani endelevu nchini Rwanda kupitia katika uchunguzi shirikishi, uimarishwaji wa utamaduni wa mjadala na mazungumzo katika masuala yanayohusiana na amani na ushirikianaji wa hali walizopitia watu mbalimbali katika uanzilishi mbalimbali wa amani.

Kwa Siku ya Amani 2013, IRDP ilipanga wiki iliyosheheni shughuli zikiwemo maonyesho ya redio kuhusu wajibu wa elimu katika ujengaji wa amani, mashidano ya kitaifa ya sanaa na uanzilishwaji rasmi wa mradi wa mazingira katika Chuo kikuu cha ASPEJ mjini Rwamagana (Mashariki). Kwenye Siku kubwa ya Amani, siku ilisherehekewa kwa kushirikiana na tume ya Umoja wa Kitaifa na Maridhiano (NURC) hafla ambayo ilijumuisha onyesho la redio la moja kwa moja lililoendeleza mazungumzo kuhusu wajibu wa elimu katika ujengaji wa amani miongoni mwa viongozi watoaji uamuzi.

Angalia kipeperushi kilicho hapa