Menu

2007

Kama sehemu yao mojawapo ya huduma yao ya mnamo 2007 nchini Afghanistan, Jeremy na Jude waliweza kusafiri hadi Jalalabad na Kabul. Walikutana na wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, serikali ya Afghan, na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali vilevile watoto wa shule na kundi la jeshi la Marekani la ujenzi.

Kwa Siku ya Amani ya mnamo 2007, WHO na UNICEF, pamoja na Wizara Afya ya Umma, waliweza kuwapatia watoto milioni 1.4 chanjo za ugonjwa wa kupooza za monovalent P3 nchini Afghanistan kusini na sehemu nyingine zilizoteuliwa za Afghanistan mashariki. UNICEF na vijana wa kujitolea wa Chama cha Mwezi mwekundi cha Afghan waliweza kupangilia Matembezi ya Amani katika mitaa ya Herat, ikafuatiwa na mjadala wa vijana kuhusu nini kunahitajika kufanywa nchini Afghanistan ili kuleta amani ya kudumu. Kulikuwa pia na sherehe ya kurudishwa kwa silaha, maombi ya amani katika misikiti, shule zilipakwa rangi nyeupe na shughuli za kielimu. Eneo kubwa la ardhi ambalo lilikuwa tayari kwa shughuli za ukulima lilikabidhiwa kwa jumuia ya mahali hapo.

2008

Mnamo Agosti mwaka 2008, Jeremy alielekea Afghanistan, tena akiwa na balozi wa Peace One Day Jude Law, na wakaweza kukutana naye Rais Hamid Karzai, wakala za Umoja wa Mataifa na vyama vya jumuia ya kiraia. Kongamano la waandishi wa habari liliweza kufanywa na Jeremy Gilley pamoja na Jude Law, kama mojawapo ya mwito wa kuchukua hatua kwa watu waliomo Afghanistan kuzingatia Siku hii ya Amani.

Katika Siku ya Amani ya mnamo 2008, kulikuwa na punguzo kwa asilimia 70 la visa vya ukatili kwenye Siku ya Amani kufuatia ahadi zilizotolewa na Rais Karzai wa Afghanistan na majeshi ya Umoja wa Mataifa katika siku ya kutokuwa na ukatili.

UNICEF, WHO pamoja na Wizara ya Afya ya Umma waliweza kuchanja watoto milioni 1.6 dhidi ya ugonjwa wa kupooza kama mojawapo ya kampeni ya Siku ya Amani ya 2008.

2009

Mnamo mwaka 2009 kiwango na kipimo cha shughuli za Siku ya Amani kiliongezeka, huku kushiriki kukiwa kwingi kutoka jumuia ya kiraia na mashirika mingine na Mashirika yasiyokuwa ya Serikali kama vile Oxfam na War Child. Kutokana na mikataba ya Siku ya Amani iliyowekwa na wahusika wote katika eneo wakala za Umoja wa Mataifa na serikali waliweza kuendelea na kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa kupooza katika Siku ya Amani, pamoja na shughuli nyingine muhimu.

Kabla ya Siku ya Amani ya mnamo 2009, Serikali ya Afghanistan iliweza kuamuru majeshi yake kusalimu amri. Azimio sawa na hilo la kusitisha operesheni liliweza kutolewa na ISAF. Taliban nao walikubali kusaidia shughuli hiyo ya chanjo ya ugonjwa wa kupooza katika Siku hiyo ya Amani iliyoandaliwa na serikali ya Afghan pamoja na wakala za Umoja wa Mataifa, kwa kukariri kwamba wazingedhuru au kuzuia wafanyakazi wa afya 14,000 na wale wanaojitolea waliohusika katika kampeni ya Siku ya Amani.

Karibu watoto milioni 1.2 wa Afghani walifaidika kutokana na chanjo hii ya ugonjwa wa kupoza katika mikoa minane, zikiwamo sehemu ngumu zaidi kifikiwa kama vile Kandahar, Uruzgan, na Helmand.

Shughuli hiyo ya kampeni ya chanjo ya kupooza kwa watoto ni jitihada za pamoja za mamlaka ya afya za Afghan, WHO na UNICEF, pia iliungwa mkono na washiriki mbalimbali wakiwemo Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya afya.

“Hii ni bora zaidi kuliko mzunguko wowote wa chanjo ya Afghanistan katika miezi 18 iliyopita,” alisema Peter Graaff, Mwakilishi wa WHO Nchini humo. “Tunayo furaha kubwa kwani kuweza kufuatiliwa namna hii kunatupatia fursa bora zaidi kuliko ile tuliwahi kuwa nayo ya kukomesha ugonjwa wa kupooza,” aliongezea.

Mnamo Septemba 21, UNAMA ilitangaza kuwa kutakuwa na usitishwaji wa nadra wa muda wa saa 24 wa operesheni vamizi za kuadhimisha Siku ya Amani ya Kimataifa zilionekana kukita mizizi kote Afghanistan, huku kukiwa na makukio ya hapa na pale ya usalama ambayo yaliripotiwa kufikia mwishoni mwa alasiri. Maafisa kutoka Wizara ya Ulinzi Afghanistan na Jeshi Saidizi la Kimataifa la NATO lilisema kwamba siku hiyo ilionekana tulivu kuliko kawaida (chanzo: UNAMA.)

Huduma Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) iliweza kuendesha kampeni kuu kwenye TV na redio kwa mwenzi mmoja iliyoanza mnamo Agosti 21 ikiwa na mada  “NINI UNAFANYA KWA AJILI YA AMANI?” na iliweza kuyaweka mabango makubwa 74 kuhusu Siku hiyo ya Amani kote nchini.

Kutokana na hayo jitihada za kampeni za UNAMA mnamo Septemba 22, zaidi ya watu 1,000 waliosisimukwa na furaha walikuwa wanapeperusha bendera za Siku ya Amani huku wakisubiri kwa hamu na ghamu kutoka kwa baadhi ya waimbaji maarufu zaidi wa Afghanistan katika Bustani ya Babur ya kihistoria jijini Kabul.

UNICEF ilihusika pia katika kambi ya siku-2 ya kriketi na watoto 50 wasiojiweza na warsha ya siku tatu ya kupaka ya watoto wanaorandaranda barabrani nchini Kabul.

Mnamo Septemba 21, kulikuwa na mashindano ya tiara mjini Kabul, Herat, Jalalabad, Mazar e Sharif.

Shughuli za Siku ya Amani ziliandaliwa na War Child ya Uholanzi.

Makundi ta OXFAM nchini Afghanistan yalisaidia mseto wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya nchi na kitaifa 13 yaliyoongozwa na shirika la vyomba vya habari la SABA ili kusherehekea Siku ya Amani katika mikoa 16 kote nchini. Mashirika yasiyokuwa ya serikali yaliyo na utalaamu mbalimbali (mawasiliano, ujengaji wa amani na usuluhishi wa migogoro, upigaji kampeni) walikuja pamoja katika kutilia mkazo mkakati wa ujengaji wa amani wa kitaifa, kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa.

Oxfam iliunga mkono hadharani kampeni hii ya kitaifa katika kiwango cha kimataifa, kupitia katita tovuti na anwani zao za vyombo vya habari. Walilenga zaidi katika umuhimu wa kupatia sauti wananchi wa Afghanistan na kuyaweka mahitaji yao na masilahi yao kipaombele katika mazungumzo yao.

2010

“Katika mwaka ambapo vurugu ilishamiri habari nchini Afghanistan, UNAMA inatafuta kuimarisha sauti za wananchi wachanga wa Afghanistan ambao wanashulikia suala la amani katika jumuia mbalimbali”
—Kieran Dwyer, Mkurugenzi wa kundi la mawasiliano la UNAMA

Mnamo mwaka 2010, Umoja wa Mataifa  nchini Afghanistan kwa mara nyingine uliweza kuongoza njia, huku UNAMA ikizindua kampeni yake ya Siku ya Amani Septemba 1 kwa kutumia sehemu mbalimbali za vyombo vya habari. Huku zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wa Afghanistan ikiwa chini ya miaka 25, vijana ndio walilengwa katika shughuli mbalimbali kutoka sekta zote za jumuia.

Kwa mwaka wa nne, wakala za Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan zilishughulika kuokoa maisha katika Siku ya Amani. Wakala za Umoja wa Mataifa zilishirikiana na idara ya afya ya serikali kwa kuwapa chanjo watoto 50,000 na wanawake walio na umri wa kuzaa watoto kutoka katika maeneo ya hatari-kuu dhidi ya magonjwa hatari. Kwa kuongezea hayo, kampeni ya nchi nzima ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza iliyolenga watoto milioni 8 ilizinduliwa.

Ikiwa sehemu ya kauli yake katika Siku ya Amani, Rais Hamid Karzai alitangaza kuwa imeanzisha baraza la amani linalolenga katika kutafuta njia za kudumisha amani katika nchi hio.

Mediothek – jumuia ya kiraia – kwa kushirikiana na UNAMA na wakfu wa Utamaduni wa Afghanistan na Mawasiliano ya Vyombo vya Habari (ACMCF) iliweza kupangilia shughuli mbalimbali katika Mkoa wa Kunduz. Zaidi ya maafisa 50 wa vyeo-vya-juu, wasomi wa kidini, wanahabari, wawakilishi wa vyama vya vijana na pia watoto pia walihudhuria hafla hiyo.

Mechi ya kandanda kati ya timu mbili za Kunduz ziliandaliwa, ambayo pia iliweza kupata msaada kutoka MACCA (Programu ya Kuchukua Hatua Migodini Afghanistan). Aidha, afisa wa serikali ya Kunduz waliweza kuanzisha rasmi timu ya vijana ya kandanda iliyoitwa “Timu ya Amani ya Vijana Chipukizi wa Kunduz”, ambayo ilianzishwa na ACMCF.

Kina mama wa Afghanistan walihudhuria tamasha ya Siku ya Amani Mazar-e-Sharif, mkoa wa Balkh. Mwimbaji, mtunzi, mwanaharakati wa amani na haki Farhad Darya alitumbuiza katika tamasha hiyo.

Skateistan, shule ya ushirikishi wa kielimu ya skateboarding nchini Afghanistan aliwaalika wake na wengine katika hafla hii ya Siku ya Amani. Zaidi ya wanafunzi 200, wazazi, wanariadha wachanga, Wafanyikazi wa Kamati ya Olimpiki na na wajumbe wote waliweza kuja pamoja kuzungumzia amani na ni vipi michezo inaweza kuunganisha watu.

Katika hafla hii Qur’an ilisomwa, nyimbo za amani, video, mashairi, maombi na filamu fupi inayoitwa“Mama Amani” iliyoonyeshwa na wanafunzi wa Skateistan. Hafla hiyo pia ilijumuisha pia maonyesho ya michezo skateboarding, taikondo, karate, wanasarakasi na kandanda. Kwenye hafla hii kulikuwa pia na hotuba kuhusu amani kutoka kwa Freshta Farrah, Naibu Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Afghanistan (ANOC), na Oliver Percovich, Mkurugenzi Mkuu wa Skateistan.

Katika Siku ya Amani, Vijana wa Kiafghani wanaojitolea Amani waliungana na Douglas Mackey & Dennis Mills wa Ushirika wa Maridhiano wa Marekani na John Silliphant ya Marafiki Bila Mipaka, ili kuungana pamoja kwa simu na marafiki kutoka nchi 20 tofauti na kuuliza“Kwa nini si upendo?” Vijana wa Kiafghani waliweza pia kushiriki katika kutembea kwa Amani kwa UNEP mjini Bamyan, kwa wakichangia kwa kubeba mabango yaliyochorwa na kuandikwa neno amani katika lugha 44 tofauti.

Mjini Kabul, tamasha ya Siku ya Amani iliweza pia kuandaliwa karibu na Kaburi la Nadir Shah kwenye mlima juu kabisa ya jiji. Kulikuwa na mikusanyiko ya watoto waliokuwa wakijifunza kuhusu amani madarasani, sanaa, muziki na michezo. Katika hali ya tamasha watoto walipeperusha bendera za amani au kupeperusha tiara arijojo ili kuonyesha matumaini yao. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ZahirAzimi alihudhuria hafla hiyo.

Ujumbe wa amani na maridhiano uliangaziwa na Programu ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa (UNEP) na Kamati ya Amani ya Bamyan kwa matembezi ya Siku ya Amani kupitia Milima ya Kati ya Afghanistan Mkoani Bamyan. Muziki wa amani na uigizaji vya nchini vilionyeshwa na vijana na watoto; sanaa ya mikono na  maonyesho ya uondoaji wa vilipuzi  vyote viliweza kupangiliwa. Kulikuwa pia hotuba kutoka kwa Gavana wa Mkoa wa Bamyan, HabibaSorabi, na wawakilishi wa Wizara ya Kilimo, Unyunyizaji maji na Mifunyo (MAIL), Wakala wa Kitaifa wa Kulinda Mazingira (NEPA), Idara ya Vijana na UNEP, vilevile na viongozi wa jumuia wa nchini.

Zaidi ya vijana 500 kutoka sehemu tofati za mkoa wa Nangarhar walihusika katika shughuli tofauti za amani, zilizoandaliwa na Idara ya Vijana, na kusaidiwa kikamilifu na UNICEF. Kulikuwa vilevile na mazungumzo ya meza dura ya redioni na Runingani kuhusu umuhimu wa amani; mashindano ya mashairi na uchoraji; pamoja na vinyang’anyiro vya michezo.

Wakala wa Wakimbizi wa UN – UNHCR – mjini Jalalabad pia ulipangilia hafla, hususani mechi za kriketi kwa ajili ya wale waliorudishwa na wakimbizi wa ndani (IDP), katika mikoa ya Nangarhar na Laghman.

Wasichana wa shule wa Afghan walibeba mabango katika Siku ya Amani huku wakitazama mechi ya mpira wa wavu katika shule ya wasichana ya Herat, iliyopangiliwa na UNAMA pamoja na idara ya elimu ya Herat.